AY aendesha kampeni ya kuwaomba watu wampigie kura Prezzo

 

Rapper Ambwene Yesaya ambaye ni mshikaji wake wa karibu na Prezzo, anaendesha kampeni kali kwenye mtandao wa Twitter, akiwaomba watu mbalimbali wampigie kura Prezzo ambaye ametajwa kwaajili ya elimination ya Big Brother Africa wiki hii.

“KEEP PREZZO IN THE BBA HOUSE RT TO THE WORLD,” ametweet na kuwaomba wasanii wenzake kufanya hivyo pia kwa wale wanaowafollow kwenye Twitter.

 

Prezzo anahitaji kura zaidi kutoka kwa watu wa Afrika Mashariki kwakuwa Afrika Kusini na nchi za Afrika Magharibi zimeungana kuendesha kampeni ya chuki ili Prezzo asishinde.

Sababu ya Afrika Kusini kumchukia Prezzo ni jinsi alivyokuwa na maelewano kidogo na mshiriki wa nchi hiyo Barbz ambaye ameshatoka.

Wanaijeria wanamchukia Prezzo kutokana na dharau zake na jinsi anavyoumiza moyo wa Goldie ambaye anampenda kwa dhati.

Kama watu wa Afrika Mashariki hawatampigia kura za kutosha, wiki hii inaweza kuwa mwisho wa Prezzo kuiwakilisha Kenya na kufuta matumaini ya kwenda kwao na kitita cha dola 300,000.

AY na Prezzo waliwahi kufanya ngoma ya pamoja iliyohit sana ya 'Nipe Nikupe'.

 

Tags:

| |