BBA: Mkenya (Dj Joe Mfalme) na Mnaijeria (Davido) kukinukisha kesho

 

Dj maarufu wa nchini Kenya anayefanya mambo yake kupitia Capital Fm, Dj Joe Mfalme anatarajia kuwarusha wapenda burudani watakaohudhuria live eviction show,kesho.

Dj Mfalme atakuwa kwenye 1 na 2 wakati staa chipukizi wa Nigeria Davido akipanda kwenye stage kuwarusha raia kwa performance ya nguvu.

Davido yupo juu sana sasa hivi nchini Nigeria na Afrika kwa ujumla na ngoma yake yenye bonge la video iitwayo Ekuro. Pia amewahi kutamba na ngoma kama Back When akiwa na Naeto C na nyingine iitwayo Dami Duro.

Kesho ndo siku ambayo hatma ya mfalme wa Bling kutoka Kenya,Prezzo itajulikana kwakuwa ni miongoni mwa washiriki waliotajwa kutoka.

Kura za wanaafrika mashariki ndizo zitakazomwokoa kwakuwa watu wa Afrika Magharibi na Kusini wanamchukia kama kirusi.