Beyonce amkaushia Kim Kardashian kwenye BET Awards

Bila shaka baada ya kuziona picha za Beyonce na Kim Kardashian wakiwa pamoja na mabwana zao, Jay-Z na Kanye West utakuwa umefikiria kuwa akinadada hao sasa wamepatana! Ukweli ni kwamba bado Beyonce hamkubali Kim kama rafiki.

Issue ni kwamba Beyonce anadaiwa kumlia buyu Kim Kardashian licha ya kukaa pamoja.

 

Beyonce siku hiyo alikuwa amekaa jirani na mdogo wake Solange Knowles mumewe Jay-Z, wakati Kanye West alikuwa amekaa baada ya partner wake wa Watch The Throne Jay-Z na kumwacha Kim pembeni.

Kim mwenye miaka, 31 alionekana kutokuwa comfortable karibu muda wote wa show hiyo na alikuwa haunganishwi kwenye story za wengine kwenye kundi hilo.

Bey na Kim waliongea mara moja tu na muda mwingine uliosalia hakuna story zozote zilizoendelea kati ya warembo hao!

Chanzo kimoja kimeuambia mtandao wa HollywoodLife kuwa Bey alimkaushia Kim kwa makusudi.

 

Bey noma hivyo bana!