Big Sean na Meek Mill waizungumzia Diss ya Breezy kwa Drake

Saa kadhaa baada ya Chris Brown kuachia ngoma ya kumdiss Drake kwenye internet kwa freestyle katika track ya The Game iitwayo "I Don't Like", rappers Big Sean na Meek Mill wametoa maoni yao.

Kwake Big Sean, freestyle mpya ya Breezy imethibitisha kuwa si msanii wa R&B pekee bali ni mchanaji haswaa.

"Hiyo ndo burudani kwenye hip hop  nayoiona,” Sean alisema kwenye interview aliyofanya na Miss Info. "Watu hawamjui  Chris Brown, lakini ni mshkaji wa ukweli. Ni mgumu pia. Sio laini ama kitu gani… Ni mgumu. Ni miongoni mwa washkaji waliobadilika sana. Anarap, anaimba, anacheza ... [Nani anashinda?] Sijui. Siwezi hata kujudge, kweli. Kwangu, Chris ni mwanangu na haijaniathiri , hiyo ni burudani, nataka tu kuona wapi itaelekea. (Miss Info TV)

Kwa upande wake Meek Mill alipoulizwa anaionaje freestyle hiyo amesema, "Nimeisikiliza, sio deep kivile. Ninatumaini kuwa wataachana nayo. Kila mmoja anapata hela, wafanye mambo yao. Wawaachie hiyo kwa watu wasio na hela.”