Diamond atoa ujumbe mzito kuhusiana na mama yake

Diamond anafahamika kwa jinsi alivyo karibu na mama yake. Kupitia Instagram jana msanii huyo amepost picha akiwa karibu na mama yake huyo na kuandika:

"Vingi unaweza kuvipoteza na ukavipata vingine, lakini Kamwe huwezi kupata Mama Mwingine... hivyo Tuwapende na Kuwaheshim sana Mamazetu kwani siku tukiwapoteza hatuto pata mwingine kamwe! Na hata vitabu tukufu vinatuambia Pepo ziko chini ya nyayo za wazazi wetu... Nakupenda sana Mama angu... Mama Nasibu."