Diamond: Niko ‘booked’ hadi mwezi July

Staa wa Mbagala, Diamond Platnumz jana kupitia kipindi cha XXL cha Clouds FM alizungumzia masuala kadhaa yaliyokuwa yakisemwa juu yake likiwemo lile la kuwa siku hizi show zake zimeishiwa mashabiki.

Akijibu kuhusu suala hilo, Diamond alisema, “mtu anasema yeye ananiroga mimi nashuka mwezi mzima ntakuwa na show Europe, Jumamosi nina show Hyatt pale, Jumapili nina show Mombasa wiki inayofuata ninasafiri naenda nje nina show kama kumi  yaani ukinibook mimi mpaka mwezi wa saba nimejaa wewe unaniambia mimi nimeshuka vipi.”

Diamond ndio msanii anayetafutwa zaidi kwa sasa na waandaji wa show ndani na nje ya nchi.