Jay-Z, Kanye West na Beyonce watawala tuzo za BET

 

Blue Ivy Carter ana uhakika wa kupata ‘vidude’ viiiingi vinavyong’aa vya kuchezea akiwa peke yake.

Tuzo za BET zimefanyika alfajiri ya leo mjini Los Angeles na walioibuka na ushindi zaidi ni pamoja na Nicki Minaj, Kanye West, na of course, Mr and Mrs Sean Carter (Jay-Z na  Beyoncé).

 

Kanye aliyekuwa ametupia pamba za white juu mpaka down, aliungana na rapper 2 Chainz na baadaye na mshindi wa Best New Artist Big Sean kuperform ngoma yao inayohit kwa sasa, Mercy.

Kanye aliongoza na mpenzi wake Kim Kardashian na walikaa siti za mbele kabisa jirani na Jigga na Bey.

Show yenyewe ilikuwa ikiongozwa na muigizaji Samuel L. Jackson ambaye yeye na muongozaji wa filamu Spike Lee waliimba version ya utani (parody) ya wimbo wa Kanye na Jigga Niggas in Paris.

 

Performance nyingine imetoka kwa Usher, Nicki Minaj and 2 Chainz, Melanie Fiona, D’angelo(!), Rick Ross na wana Maybach Music Group, bila kumsahau Chris Brown.

 

Show hiyo pia ilitumika kumuenzi Whitney Houston ambapo wasanii kadhaa waliimba nyimbo zake akiwemo Monica, Brandy (walioimba “I’m Your Baby Tonight” na  “I Wanna Dance With Somebody”), mama yake Whitney,Cissy Houston (aliyeimba  “Bridge Over Troubled Water”), na Chaka Khan, aliyeimba “I’m Every Woman.”

 

Hi indo list nzima ya washindi wa tuzo hizo:

Best Group: The Throne (Kanye West & Jay-Z)

Best Actor: Kevin Hart

Best New Artist: Big Sean

Best Male R&B Artist: Chris Brown

Best Collaboration: Wale ft. Miguel

Best Gospel: Yolanda Adams

Best Female R&B Artist: Beyoncé

Best Female Hip-Hop Artist: Nicki Minaj

Lifetime Achievement Award: Maze featuring Frankie Beverly

Video Of The Year: “Otis,” The Throne (Kanye West & Jay-Z)

BET Humanitarian Award: Rev. Al Sharpton

Viewers’ Choice Award: Mindless Behavior

Video Director Of The Year: Beyoncé & Alan Ferguson

AOL Fandemonium Award: Chris Brown