Justin Bieber azitosa tuzo za Uingereza kwa kwenda shopping na Will.i.am

JUSTIN BIEBER  alizitosa tuzo za Uingereza (Brits Awards) jana usiku na kwenda kufanya shopping na will.i.am.

Mashabiki wa Uingereza wa staa huyo walikuwa wakimtegemea kumuona live kwenye tuzo hizo kubwa za Uingereza.

Lakini hata hivyo wakati Justin Timberlake, Muse na Emeli Sande  walikuwa wakitumbuiza kwenye eneo la O2,  msanii huyo wa Canada alikuwa nje akifurahia shopping.

Mashabiki wa Bieber waliumizwa na kitendo hicho na kuamua kuutumia mtandao wa Twitter kulalamikia kitendo cha staa huyo kutokuwepo kwenue show hiyo ya live.

Shabiki mmoja wa Justin Bieber aliandika : "I'm not even bothering to watch the Brits 2013 bc no Bieber."

Mwingine aliongeza: "No I don't want Justin Timberlake I want Justin Bieber, brits sort it out."