Kanye West audiss wimbo wa Justin Timberlake aliomshikisha Jay-Z, 'Suit & Tie'

Kanye West ameudiss wimbo wa Justin Timberlake uitwao Suit and Tie aliomshirikisha Jay-Z na kusisitiza kuwa haupendi.

Timberlake alivunja ukimya wake wa miaka sita bila kutoa ngoma mwezi uliopita kwa kuachia wimbo huo na pia mapema mwezi huu yeye na  Jay-Z  waliperform pamoja kwenye tuzo za Grammy.

Mastaa hao sasa wanatarajia kufanya ziara ya pamoja iitwayo Legends of the Summer  lakini Kanye anaonekana kutopendezwa na muungano huo kwa kuamua kuuponda alipokuwa kwenye concert jijini London.

Kwenye video ambayo mtandao wa TMZ imeipata, Kanye aambaye ni swahiba wa karibu wa Jay-Z alisikika akiuambia umati uliokuwa ukimtazama "I got love for Hov (Jay-Z), but I ain't f------ with that Suit & Tie."