Mariam Khamis wa TOT Taarab afariki dunia

Wapenzi wa muziki wa taarab nchini Tanzania wapo kwenye majonzi kwa kumpoteza muimbaji mahiri wa muziki huo Mariam Khamis.

Mariam amefariki jana usiku katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam wakati akijifungua lakini mwanae ni mzima.

Marehemu Mariam amewahi kuimba nyimbo nyingi zikiwemo 'Paka Mapepe, Uzushi Wenu Haunitii Doa na Sidhuriki na Lawama, ‘Huliwezi bifu’, ‘Raha ya mapenzi’ na ‘Ndo basi tena’

Makundi aliyowahi kufanya nayo kazi ni pamoja na  Zanzibar Modern Taarab, Five Star na baadaye TOT.

Mungu ailaze roho ya marehemu Mariam mahala pema peponi. //JanB Multimedia