Mume wa Goldie anyimwa visa ya kwenda Nigeria

Mipango ya Andrew Harvey – mume wa marehemu Goldie kuhudhuria mazishi ya mkewe weekend hii inaweza kukwama kutokana na ubalozi wa Nigeria nchini Uingereza kumtosa visa ya kuingilia nchini humo.

Hata hivyo mkandarasi huyo wa Uingereza aliyemuoa mwanamuziki huyo aliyefariki ghafla wiki iliyopita mwaka 2005, amepanga kuomba visa kwenye ubalozi mwingine ili aweza kuhudhuria mazishi.

Katika hatua mtandao wa The DAILY POST wa Kenya umethibitisa kuwa Prezzo aliwasili jana usiku jijini Nairobi akitokea Nigeria na kuviambia vyombo vya habari kuwa hayupo tayari kufanya mahojiano.

Alidai kuwa siku ya mazishi haijapangwa bado na hivyo aliamua kurejea nyumbani.