Mwana FA afuata nyayo za AY kwa kuanzisha kampuni

Rapper Hamis Mwinjuma aka MwanaFA ameamua kuutumia ukongwe wake kwenye muziki kwa kuanza kusaidia wasanii chipukizi ambao watakuwa chini ya kampuni yake ya Life Line Inc.

Hivi karibuni hitmaker huyo wa Bado Nipo Nipo amemchukua msanii wa kike aitwaye Maua Sama ambaye ametoa wimbo wake wa kwanza redioni uitwao So Crazy.

“Niliona naweza kutoa mkono sasa, nimefanya muziki kwa muda mrefu na siwezi kumsaidia kila mmoja anayefanya mziki. Kuna watu wanavipaji vinapotea mtaani huku, na nikaona naweza kufanya kitu, kwahiyo tutakuwa very selective, maana hatutaki kuwa na watu wengi kwenye lebo tukashindwa kusambaza kazi zao,” Mwana FA ameiambia blog ya Dj Fetty.

“Tutachagua wawili watatu ambao tutaona vipaji vyao vinajitosheleza na kuwasimamia haitatupashida.Maua ndio ameanza sema kuna wengine wawili watatu mnawajua ila Maua tumeona ndio wakati wake, na muda haujafika wa sisi kuwataja na kuanza nao kazi rasmi hadharani, bado tunafanya kichinichini.”

Aliongeza, "lebo ina kama mwaka hivi lakini tunaendesha shughuli kichinichini, tunajaribu  ku scout watu, kupanga mambo yetu, kusajili kampuni yaani utaratibu wa nyuma kabla muziki haujaskika.”