Rihanna atajwa ‘Mwanamke wa Mwaka’ wa jarida la Vogue

 

Mwanadada Rihanna aka RiRi ametajwa na jarida la Vogue la nchini Italia kama Mwanamke wa Mwaka.

Mrembo huyo amewapiga fimbo mastaa wengine wakubwa duniani katika tuzo hiyo kutoka kwa jarida hilo lenye heshima kubwa duniani akiwemo Lady Gaga.

 

Vogue limesema uamuzi wake wa kumpa tuzo Rihanna anayetamba sasa na kibao 'Where Have You Been' ni kwasababu ya ukarimu wake.

Hata hivyo wapo wanaopinga Rihanna kupewa tuzo hiyo kutokana na baadhi ya scandal zinazomwandama ikiwa ni pamoja na uvutaji wa bangi hadharani.