Solothang amchana Miss Tanzania kicheche

 

Msafiri Kondo aka Solothang leo ameachia ngoma yake mpya iitwayo Miss Tanzania iliyotengenezwa na producer wa Tongwe Records J-Ryder.

Katika wimbo huu Solothang anamzungumzia msichana mrembo aliyewahi kuwa Miss Tanzania lakini tabia zake za ukicheche zinamharibia.

 

“Kinachomponza huyu shorty  utulivu sifuri, ila hakuna anayepinga huyu demu ni mzuri” ni mstari unaobeba maudhui yote ya wimbo huu.

Anazungumzia jinsi msichana huyo anavyotembea na vigogo na amegeuka mama huruma.

 

Ni wimbo ambao umebeba ukweli kwa baadhi ya mamiss Tanzania wa zamani ambao kila kukicha wamekuwa wakiandikwa na magazeti kwa scandal mbalimbali.

 

Miss Tanzania ni ngoma yake ya sita kutoka kwenye album yake I AM TRAVELLAH VOL 1 ambayo ina jumla ya nyimbo  nyimbo 14.

Solothang amesema video ya wimbo huu itafuata  jumamosi ijayo.

 

Kwa sasa albam yake inapatikana kwenye soko la mtandaoni (itunes) ,tesco,spotify,emusic na kwingineko.

Download ama kusikiliza wimbo huo hapa:

www.4shared.com/mp3/XUFqJ6Gr/MISS_TANZANIA_1_.html?