Tarrus Riley kupiga show Nairobi, Kenya

 

Mwanamuziki wa reggae aishiye Marekani lakini mwenye asili ya Jamaica, Tarrus Riley anatarajiwa kupiga show nchini Kenya mwezi wa August.

Hiyo itakuwa ni ziara ya kwanza barani Africa na atakuwepo huko kwenye tamasha la kimataifa la “Big Tuners Festival of Music"

Msanii huyo amehit na ngoma kama "Protect the People", "She's Royal", "Getty Getty No Wantee", na "Armaggedeon.

Tarrus Riley alizaliwa kwa jina la Omar Riley, 1979 huko The Bronx, New York City, Marekani.

Ni mtoto wa mwanamuziki wa reggae wa Jamaica Jimmy Riley..