Tigo Tanzania yatajwa kuwa brand inayofanya vizuri kwenye Facebook duniani

Tigo Tanzania imetajwa kuwa ni miongoni mwa brand za juu duniani zinazojituma zaidi kwenye mtandao wa Facebook kutokana na ripoti iliyotolewa na SocialBakers tarehe 7 February 2013. Ripoti hiyo ilikuwa ikiangalia makampuni 10 duniani yanayojituma zaidi kwenye Facebook katika kipindi cha robo ya  mwisho ya mwaka jana.

Tigo Tanzania ni kampuni pekee ya simu kutoka Afrika Mashariki, Kati na Kusini kwenye orodha hiyo ikijumuika na makampuni makubwa duniani.

"Tigo Tanzania  imekamata nafasi ya nane kwenye chart kwasababu ya kujituma kwake katika kuwahudumia wateja. Tunawathamini wateja wetu sana na kuwekeza zaidi kuhakikisha kuwa tunakuwepo muda wote wanapotuhitaji,” alisema  brand manager wa Tigo.

Tigo inadaiwa kuwa na asilimia 87.30%  ya uharaka wa kuhudumia wateja.