Tyrese, Ginuwine, na Tank waunda kundi, wamponda Usher na wengine kwa kuiharibu R&B
Muimbaji na muigizaji Tyrese Gibson ameonekana kuwarushia madongo wasanii wenzake akiwemo Usher na Chris Brown walioperform kwenye tuzo za BET kwa namna walivyoubadilisha muziki wa R&B.
Usher alitumbuiza kwa wimbo wa 'Climax' kwenye tuzo hizo zilizofanyika alfajiri ya leo kwa saa za Afrika Mashariki, wimbo uliopo kwenye albam yake ya Looking 4 Myself.
Hata hivyo mtu mmoja ambaye hajapendezwa na performance hiyo iliyosifiwa na wengine kutokana na uimbaji mpya wa Usher, ni Tyrese,anayedai kuwa R&B ya ukweli ipo kwenye kundi lake linaloundwa na yeye, Tank na Ginuwine.
"Hatuna house, hatuna techno...tunakuja na R&B ya ukweli," Tyrese aliandika kwenye Twitter.
“R&B imeharibiwa. Tunakuja kuwakumbusha nyote kwanini mlipenda muziki wa RNB. TGT inakuja siku si nyingi."