Video ya Addicted ya Hussein Machozi kutoka wiki hii

 

Mwanamuziki wa Tanzania ambaye mara nyingi anaishi nchini Kenya Hussein Machozi ataachia video ya wimbo wake mpya Addicted wiki hii.

Video hiyo imefanyika nchini humo na kampuni ya Ogopa Dj.

Machozi ambaye amedai kuwa muziki wa Tanzania umejaa majungu na upendeleo amesema , “wacha tuwaachie wananchi ambao wamezoea kulazimishwa kupenda visivyo na haki ya kupendwa,” akimaanisha kuwa video hiyo ikitoka wananchi ndio watakaoamua kuipenda ama lah!

 

Hivi karibuni alidai kuwa anapenda kufanyia muziki nchini Kenya kwakuwa huko muziki mzuri huchezwa bila kujali ni wa nani  ambapo wao huzingatia kipaji cha mtu.

Aliongeza kuwa Tanzania imetawaliwa na radio moja ambayo ni kama inautawala muziki wa Bongo na radio zingine kutokuwa na msimamo wa kweli.

Pia alisema anafikiria kuhamia kabisa nchini Kenya panapo majaliwa.