Zitto Kabwe aiomba serikali kuwasaidia wasanii dhidi ya unyonywaji wa jasho lao
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe ameiomba serikali ya Tanzania kuhakikisha kuwa inachukua hatua mahsusi za kulilinda jasho la wasanii.
Zitto ambaye hivi karibuni amejichukulia sifa nyingi kwa kuwezesha kuundwa kundi la wasanii wenye asili ya mkoa wa Kigoma, 'Kigoma All Stars' amesema hayo kwenye mtandao wa Twitter.
‘Wasanii wetu wananyonywa sana. Naamini Serikali itachukua hatua mwafaka kuhakikisha kila msanii anafaidika na kazi yake,’ alitweet.
Katika hatua nyingine mbunge huyo na wasanii wa Kigoma All Stars wameendelea na maandalizi ya show ya July 17 mwaka huu itakayofanyika mkoani Kigoma kwaajili ya kukusanya fedha kusaidia wasiojiweza.
Leo (July 13) akinadada Mwasiti, Darleen na Recho wamerekodi wimbo uitwao Ningekuwa kwetu Mirumbani.