50 Cent alitetea penzi la Rihanna na Chris Brown

50 Cent amewatetea Chris Brown na Rihanna walioamua kurudiana na kusema kuwa watu waache kumsonga Chris kwa kumpiga Rihanna mwaka 2009.

Muimbaji huyo 'Diamonds' Rihanna aliliambia jarida la Rolling Stone, kuwa yeye na Chris wameruadiana na kusema kuwa uamuzi wake wa kumrudiana utakuwa ni kosa lake mwenyewe. Pia alisema Chris haonekani kama atarudia kosa lake tena.

50 Cent anaamini kuwa Chris Brown angeachwa sasa kuadhibiwa kwa kumpiga Rihanna na kwamba tayari ameshalipa kwa kufanya kitendo hicho.

“It’s in the past. How long do you have to pay for a mistake you made?” 50 aliliambia Daily Star.

“When your debt is done, it’s been paid to society. Rihanna is doing her thing.”