50 Cent kupiga show Uganda mwezi September

Rapper Curtis Jackson aka 50 cent ambaye juzi alipata ajali ya gari nchini Marekani, anatarajiwa kupiga show mjini Kampala, Uganda, mwezi September mwaka huu.
Rapper huyo atatumbuiza katika maadhimisho ya miaka 50 tangu uhuru wa nchi hiyo.
Hii si mara ya kwanza kwa 50 kuja Afrika Mashariki. Alishaitembelea Kenya na Somalia akiwa na shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia masuala ya chakulan duniani, WFP, mapema mwaka huu ili kushuhudia madhara ya njaa katika nchi za pembe ya Afrika.
Ana mpango wa kutoa milo bilioni moja kwa watoto wenye njaa katika kipindi cha miaka mitano.
Kila ‘nunuzi’ la Street King, kinywaji anachokipromote rapper huyo, litatoa mlo mmoja kwa mtu mwenye uhitaji kupitia shirika laa mpango wa chakula duniani.
50 Cent alisema aliguswa na watoto aliowatembelea huko Kibera, Nairobi nchini Kenya. Alisema watoto hao walikuwa hawana habari ya maisha magumu na ya hatari waliyonayo lakini walikuwa na nguvu na uchangamfu kama watoto wa Marekani.
Pamoja na show ya September ya 50 nchini Uganda, mwezi August wanatarajiwa kudondoka wakali wengine kama Sisqo wa Dru Hill na wajamaica Demarco na Wayne Wonder.

SOURCE: https://www.bongo5.com