Aika na Nah Reel wajitoa kwenye kundi la Pahone

Producer maarufu nchini na member wa kundi la Pahone na Aika wamejitoa kwenye kundi hilo. Akiongea na East Africa Radio, Aika amesema wamejitoa kwenye kundi hilo kutokana na kushindwa kuelewana kama kundi.

Aika amesema licha ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Nahreel kila mmoja ataendelea kuwa solo artist.

Amesisitiza kuwa yeye sio sababu ya kuvunjika kwa kundi hilo. Pia amesema kama msanii wa kujitegemea ataachia ngoma spesho kwa siku ya wapendanao iitwayo Usinibwage.