Avril kuachia video ya ‘Hakuna Yule’ kwenye Valentine’s Day

Mwanamuziki wa nchini Kenya Avril maarufu kwa ngoma yake Kitu kimoja, amepanga kuachia video ya wimbo wake mpya Hakuna Yule kwenye Valentine’s Day.

Akitajwa kama msanii wa kike mrembo zaidi nchini Kenya video yake inangojewa kwa  hamu na mashabiki wake.

Hivi karibuni kabla ya kutoa wimbo huo Avril aliwapa fursa mashabiki wake kumchagulia jina la wimbo.