BREAKING NEWSss: R.I.P STEVEN KANUMBA (Bongo Movie Star)

BREAKING NEWSss: R.I.P STEVEN KANUMBA (Bongo Movie Star)

Habari za ghafla zilizotufikia mida hii kutoka kwa vyanzo mbalimbali vya habari nchini Tanzania; ni kwamba, Gwiji la filamu nchini humo Steven Kanumba katutoka, hatunae tena!! Mpaka saivi maiti yake iko mochwari hospitalini Muhimbili, Habari zaidi zenye uhakika zijawajia ivi karibuni! Atakumbukwa sana kwa mchango wake mkubwa nchini Tanzania katika tasnia ya uigizaji.Mungu akulaze mahala pema peponi Kanumba 'The Great' 

Mpaka sasa taarifa ni kuwa mazishi ya Kanumba yatakuwa Jumanne tarehe 10, taratibu za kipolisi kwa kuwa kuna utata wa kifo chake pia zimefanya ratiba ziwe na utata pia. Msiba uko nyumbani kwa Kanumba, Sinza jirani na Vatican City Hotel. Habari hii ni kwa hisani ya John Kitime

Kwa habari mpya kabisa kuhusu kifo cha Kanumba tembelea hapa: https://millardayo.com/?p=9937