Chameleone ahama kwenye nyumba yake ya Seguku kuhofia usalama wa familia yake

Hivi karibuni Chameleone alikuwa kwenye uchunguzi wa tukio la mauaji kijana aitwaye Robert Karamagi aliyekufa nyumbani kwake. Mtu huyo alidaiwa kuvamia kwenye nyumba yake kwa lengo la kutaka kumuua mke wake Daniella Atim Mayanja  lakini kwa bahati mbaya alimwagia mafuta na kujichoma moto mwenyewe.

Kutokana na tukio hilo, Chameleone ameamua kuhama nyumba hiyo ya Seguku na kuhamia kwenye nyumba nyingine ya Muyenga mjini Kampala.

Kupitia Facebook Chameleone alisema, “My security and that of my family was compromised in Seguku. Therefore it was prudent to acquire another place as the security issues at Seguku got fixed. Again this will allow for the renovation work that has been going on at Seguku for the last 4 months get finished more efficiently. Leone Island family, introducing my new hut in Muyenga…”

Kwa mujibu wa meneja wa Chameleone, Sam Mukasa, nyumba hiyo ya Muyenga  ni miongoni mwa nyumba alizonunua msanii huyo chini ya kampuni yake ya ‘Chameleone Investments’.