Chris Brown aomba diss track yake ichezwe mbele ya wana YMCMB

 

Inaonekana kama story ya beef kati ya Chris Brown na Drake haiwezi kuisha leo. Kuna tetesi kuwa Chris yupo kwenye mission ya kumchokoza zaidi Drake ajibu diss yake “I Don’t Like” freestyle aliyoiachia siku chache zilizopita.

 

Baada ya tuzo za BET, Chris alienda kwenye klabu ya usiku ya Supperclub mjini Los Angeles na kumuomba dj aicheze track hiyo anayomdiss Drake.

Tatizo ni kuwa maofisa wa juu wa Young Money walikuwepo kwenye klabu hiyo akiwemo  meneja wa Lil Wayne na Drake,  Cortez Bryant na rais wa YMCMB, Mack Maine.

 

Kwa  mujibu wa vyanzo vya RumorFix ndani ya klabu hiyo, “Walicheza ngoma hiyo na Chris akasikika akifuatiliza mashairi na kurap kwa mdomo part yote; it was funny.”

 

“Young Money walikuwa  chumba kingine. Drake hakuwepo lakini meneja wake alikuwepo, pamoja na executives Mack Mane na  Cortez Bryant.  Hawakufanya chochote.

 

It's seem like Breezy kaanza uchokozi tena! Katika habari nyingine mwandishi wa mtandao maarufu wa  udaku, mediatakeout alimuuliza Drake kama amesikia diss hiyo na Drake akamjibu, "I'm not responding to that fag."