Drake akataliwa kuingia club kwakuwa Chris Brown alikuwa ndani

Club moja ya usiku huko Hollywood, Marekani ililazimika kumkatalia Drake asiingie ndani kwakuwa tayari Chris Brown alikuwa ameingia.

Vyanzo vimeuambia mtandao wa TMZ kuwa mabaunsa wa club hiyo iitwayo Playhouse walimzuia Drake Jumatano hii kuingia kwasababu Chris alikuwa akiparty ndani.

Sababu ya kufanya hivyo ni kuepusha mazingira ya wakali hao wa muziki kutwangana tena.

Kwa mujibu wa vyanzo, Brown alikuwa ndani ya club hiyo akisherehekea anniversary party ya kampuni ya nguo ya Popular Demand.

Mabaunsa hao walifahamu Chris yupo ndani hivyo baada ya Drake kuibuka na kuwa na uhakika kuwa Rihanna angejumuika pia walimuomba Drake akale bata sehemu nyingine usiku huo.

Inadaiwa kuwa Drake hakuwa mbishi kuondoka baada ya kukataliwa kuingia ndani.