Dully Sykes ajitolea kusaidia wasanii wakongwe waliopotea kwenye muziki

Msanii na producer wa Bongo Flava, Dully Sykes amesema amedhamiria kuwasaidia wasanii wenzake walioanza muziki pamoja ambao kwa sasa wamepotea.

Kwa kuanza, Dully amemchukua Inspekta Haroun ambaye atakuwa chini ya menejimenti yake na studio anayoimiliki ya 4.12. Tayari wasanii hao wameshatoa ngoma ambapo Inspekta amemshirikisha Dully kwenye wimbp uitwao Ashura.

Wasanii wengine ambao hitmaker huyo wa Utamu Utamu amepanga kuwatoa tena ni pamoja na Mack D na kundi la Manzese Crew. Akiongea na Clouds FM, Dully amesema pia kuwa hivi karibuni ataachia wimbo mpya aliowashirikisha AY na Jokate Mwegelo.