Exclusive: Floyd Mayweather Sr. kumtrain Drake ama Chris Brown kwa pambano lao

 

Kama Drake akikikubali ofa ya dola milioni 5 kuzichapa na Chris Brown, rapper huyo kutoka Canada, atapewa mafunzo na legend wa masumbwi .

Mtandao wa RumorFix umebaini kuwa promoter wa masumbwi Damon Feldman amemsainisha Floyd Mayweather Sr.  kuwafundisha Chris Brown ama Drake ili kujiandaa na mechi yao.

Mayweather Sr. of course, ni baba yake na FloydMoney Mayweather Jr.

 

Tayari Chris Brown ameshakubali kuingia ulingoni kuzichapa na Drake, kama naye akikubali vigezo vilivyowekwa.

Kama Drake akikubali, pambano hilo litafanyika September 15,tarehe iliyopangwa na Feldman pamoja na tajiri anayetoa hela hiyo Alki David.

Jamaa hao wamewaahidi Drake na Brown dola milioni 5 iwapo wakikubali kuzichapa kwenye pambano hilo litakakolofanyika jijini Las Vegas.