FAIDIKA NA JANB MULTIMEDIA

Faidika na shindano la JANB MULTIMEDIA. Kama wewe ni Mtanzania na una kipaji cha kuimba vizuri na kurap fresh katika ''new era music" na haujapata nafasi ya kwenda studio kufanya kazi ya ukweli basi tuma Demo katika ili shindano ambapo washindi wawili watapata nafasi ya kurekodi nyimbo moja katika studio mbili tofauti nchini Tanzania kwa udhamini wa JANB MULTIMEDIA. Mshindi wa kwanza atakaechaguliwa ataenda kurekodi wimbo mmoja katika studio za Dirty Mode Records-Morogoro na Mshindi wa pili atarekodi katika studio za Noizmekah Production-Arusha. Jinsi ya kushiriki; Tuma 'demo' katika email hii ;infojanb@gmail.com kisha demo zote zitasikilizwa kwa ufasaha na watayalishaji wa muziki na radio presenters wanaojua muziki wa kileo na ndio wataoamua washindi. Washindi wote wawili watapata nafasi ya kurekodi nyimbo zao katika izo studio kisha nyimbo zitafanyiwa promotion katika vituo mbalimbali vya radio kwa ajili ya kuwatangaza zaidi. Mwisho wa kushiriki ni tarehe 15/10/2012.

All the best//JanB MULTIMEDIA