FastJet yakanusha kufungiwa leseni yake nchini

Kampuni ya ndege ya Fast Jet imezikanusha ripoti kuwa imenyang’anywa leseni yake ya biashara katika nchi kadhaa barani Afrika ikiwemo Tanzania.Kupitia website yake kampuni hiyo imeandika:

Licha ya taarifa za leo kwenye vyombo vya habari, ni biashara kama kawaida hapa fastjet. Madai kuhusu kunyang’anywa leseni ni uongo mtupu.  Tunaendelea na safari zetu kutoka Tanzania na tunaendelea kuanzisha safari mpya kama ilivyopangwa.

Hii ni njama/hujuma ‘binafsi’ dhidi  ya fastjet katika jaribio la wazi lililotengenezwa kuharibu brand na sifa ya Fastjet.Ofisi zetu na matawi yetu bado zipo wazi kwa booking mpya na hakuna refund zozote.

Taarifa rasmi itapatikana masaa machache yajayo.

www.fastjet.com