Fid Q, Diamond, Chameleone, Avril na wengine kuperform kwenye ZIFF

 

Lile tamasha kubwa la Zanzibar International Film Festival, ZIFF jana limefunguliwa rasmi.

Pamoja na kuwepo na maonesho ya filamu kutakuwepo na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa Afrika Mashariki.

Waliopo kwenye orodha ya wasanii watakaoperform ni pamoja na Fid Q Atakayeperform jumanne usiku akiwa na bendi yake na kusindikizwa na mwanadada Saraha Msanii.

Wengine ni Linah, Barnaba, Diamond, Roma, Nakaaya, Carola Kinasha, Swahili Vibes na Tazneem.

Kutoka Uganda atakuwepo Jose Chameleone huku Kenya ikiwakilishwa na wanadada warembo Avril na Marya.

Wengine ni Mamadou Cissoko wa Guinea na Mama C.

Tamasha hilo litafanyika hadi tarehe 15 mwezi huu.