Frank Ocean aanika ukweli kuwa aliwahi kumpenda mwanaume mwenzie

 

Mwanamuziki wa R&B Frank Ocean ambaye wengi wamemfahamu kupitia ngoma ya Kanye West na Jay-Z ‘No Church in the Wild’ kwa kuimba chorus bomba, ameamua kuanika hadharani kuwa aliwahi kuzama kimapenzi kwa mwanaume mwenzie.

 

Kupitia mtandao wa kijamii wa Tumblr, nyota huyo amesema amependa kuzungumza fununu kuhusina na mahusiano yake ya kimapenzi.

Kwenye barua hiyo, Ocean mwenye miaka 24 ameanza kwa kuandika: "Kile nachoenda kuandika ni kwa yeyote anayejali kusoma."

"Kilikuwa kimepangwa kuandikwa kwenye sehemu ya ‘Asante; kwenye cover la albam yangu, lakini kutokana fununu zinazoendelea sasa hivi nimefikiria ni bora kuweka mambo sawa.”

 

"Miaka minne iliyopita, nilikutana na mtu, nilikuwa na miaka 19 na yeye pia.

"Tulikaa kiangazi chote na kingine tena pamoja. Tulikuwa pamoja kila siku.”

"Nilionana naye karibu siku nzima na tabasamu lake. Tulilala pamoja.

"Muda nakuja kugundua kuwa nilikuwa nampenda, ilikuwa imezidi.

"Sikuweza kutoroka, sikuweza kuzungumza na wanawake niliokuwa nao, wale niliowajali na kudhani nilikuwa nawapenda.”

Alimalizia kwa kusema, "Najua ni shujaa kwasababu ulikuwa wa kwanza. Hivyo asante."

 

Albam yake ya kwanza iitwayo Channel Orange inatarajiwa kutoka July 17.