Gari mpya ya Diamond!!

Baada ya kupiga show kibao na ambazo ofcourse zinaendelea za six figures tu, Diamond amedondosha mkoko mpya! Si gari ya kushtua sana lakini ukitaka kuinunua ni lazima ufunge kibwebwe!

 

Ama kama una hela za kubadilishia tu mboga kuipata labda uombe mkopo benki. Ni Toyota Landcruise Prado!  Tumeangalia bei kwenye mtandao tukaona bei yake inaanzia $45,000 na kuendelea. Kwa madafu inacheza kwenye milioni 70 na ushee hivi. Ukiongeza na gharama za kuifikisha Bongo huenda zikawa zimemtoka zaidi.

Hongera sana Diamond. You really needed a new toy! Let’s spin em rims and cruise!

SOURCE: Leotainment