Gentriez a.k.a Arusha Boy

 

Gentriez mwakitabu ni msanii wa Hip-Hop kutoka kundi la River Camp Soldiers jijini Arusha.Alianza mziki mwaka 2003 kupitia talent shows na free stage hasa zile za Via-Via. 2008 aliingia studio na kurekodi wimbo wake wa kwanza uliokua unaitwa ‘Mandamano Ya Haki’ ambao haukufanikiwa kufanya vizuri, then 2011 hapo ndipo nyota yake kidogo ilipoanza kuonekana. Pia wimbo huo ulikuja na mafanikio kadhaa ambapo, alipatiwa jina la Arusha boy pia akafanikiwa kufungua clothing line ya ‘Arusha boy clothing line’ chini ya Wanene Entertainment. Na sasa 2012 ameachia nyimbo yake nyingine inayokwenda kwa jina la  NNA KILA SABABU aliyomshirikisha msanii mwingine kutoka kundi la Jambo Squad, Chalii Mtoto Wa Bibi au Nigga C.. humo ndani utaskia michano mikali kama NAOTA MABAWA KWENYE MV BUKOBA KISHA NAPAA nakadhalika.Watu wakae tayari kwa ujio wa video ya wimbo huo itakayotoka hivi karibuni.Pia unaweza kusikiliza na kudownload bure nyimbo kibao zake zote alizowahi kuzifanya ONLINE kupitia: HTTP://WWW.REVERBNATION.COM/GENTRIEZMWAKITABU
 Gentriez mwakitabu mpaka sasa ameshafanya kazi na wasanii wakubwa kama  NAKAAYA,G-NAKO,BONTA,[WEUSI].DEF XTRO[NOIZMEKAH]BELLE 9, NAH REEL, MESEN SELEKTA,JORS BLES,MONA GANGSTA NA WENGINE WENGI..Gentriez Mwakitabu yuko chini ya RECORD LABEL YA WANENE ENTERTAINMENT jijini Arusha inayomilikiwa na CO-founder and C.E.O Darsh Pandit.//JanB Multimedia