Hermy, Ogopa na Rkay kupika ngoma za washiriki 10 wa TPF5

Washiriki wote 10 wa Tusker Project Fame msimu wa tano watakuwa na bahati ya kurekodi wimbo mmoja kabla ya kuondoka kwenye academy.

Nyimbo hizo zitasimamiwa na record label kubwa duniani ya Universal Music group.

Washiriki wote kumi watarekodi nyimbo hizo kwa utayarishaji wa magwiji katika muziki Afrika Mashariki akiwemo  Chris Adwar, Madtraxx, Ogopa, Rkay, Hermey B, Aaron, Tim Rimbui na Washington.

 

Nyimbo hizo zitakuwa na ladha ya Afrika Mashariki zaidi na kujumuishwa kwenye albam moja huku waandaji wa mashindano hayo wakisema kuwa mashabiki wategemee albam kali.

Mmoja wa majaji wa mwaka huu, Gerrad kutoka UMG amesema amefurahishwa na uwezo wa washiriki wengi wakati wa kurekodi.

Ingawa hiyo itakuwa ni albam ya pamoja, washiriki wote kumi, kila mmoja atanufaika kwakuwa wote watarekodi washinde, wasishinde.

 

Waandaji wa TPF5 wamesema ingawa nyimbo hizo bado hazijamilika, jinsi zilivyo nzuri inaashiria kuwa albam hiyo itakuwa moto wa kuotea mbali.

Universal Music Group mwaka huu imeungana na TPF Ili kuja kumsimamia mshindi wa mwaka huu na kumtangaza katika majukwaa ya kimataifa tofauti na mashindano ya awali.