Izzo B ashangilia kurekodiwa wimbo na Master J

Huenda Izzo B ameshafanya kazi na maproducer karibu wote wakubwa lakini si Master J. Mara zote alipokuwa akirekodi nyimbo MJ Records producer aliyefanya nyimbo zake ni Marco Chali. Jana ilikuwa ni siku ya pekee kwa rapper huyo wa Ball Player baada ya kuwa na session a kurekodi na producer huyo mkongwe, Master Jay.

“Nakushukuru mwenyezi mungu kwa kuniwezesha kurekodiwa nyimbo na @masterjtz leo tarehe 7/2/2013 siwezi sahau hii siku,” aliandika Izzo kwenye Instagram akiwa kwenye picha na Master J.