Izzo B azungumzia kuporwa demu, kutishiwa kuuliwa na kesi ya baba yake

 
Baada ya kutoka kwa wimbo wake uitwao ‘Mwaka Jana’ maswali mengi yalizuka kutokana na mambo kadhaa aliyoyazungumza kwenye ngoma hiyo. Mambo matatu makubwa ambayo wengi walipenda wapate ufafanuzi ni, kuhusu kesi ya baba yake ilivyomfanya asiendelee na chuo, kuporwa demu wake na kutishiwa kuuawa.
Leotainment imeongea naye kwa simu na hivi ndivyo alivyoelezea. 
Kuhusu kesi ya baba yake
Baba yangu alipata kesi kipindi mimi nipo chuoni. Kesi ilionekana inaweza kuisha mapema lakini ikawa tofauti. Ikaonekana inakoelekea kubaya zaidi, unajua kwenye kesi kuna kushinda na kushindwa, jinsi ilivyokuwa inaelekea ikabidi mimi mama…. Maake ilikuwa kama ngoja tu tuchune hii kesi itaisha huyu asijue sababu yupo chuo halafu na mimi nilikuwa nimebakiza kama wiki mbili nianze kufanya mitihani ya semester ya mwisho. Kesi ilivyokuwa inazidi kwenda wakaona mmh! Huku inakoelekea ni kubaya ngoja na huyu naye tumpe taarifa. Kwahiyo kitendo cha mimi kupewa taarifa, unajua kwa mtu yoyote yule inakuwa ni shock yaani kwamba baba yako yuko kwenye kesi hii iko mahakani. Kwahiyo hiyo ikaniathiri hiyo kidogo sikuweza kufanya mitihani ya semester ya mwisho, nikapostpone, nikasogeza mbele kabisa nikaona nitulie kwanza sababu mambo mengi unajua familia zetu hizi.
Kuhusu kuporwa demu
Hiyo  ni kwa kila mtu nafikiri inatokea sababu sio kwamba msanii ama mtu gani hawezi kuporwa demu sababu ukija kwenye masuala ya mapenzi au mahusiano hayajalishi wewe ni nani. Sababu hata mtoto Amber Rose alikuwa anapewa good times sana na Kanye  lakini akadata na mnyanwezi Wiz Khalifa umeona bwana! Kwahiyo hivyo ni vitu vya kawaida tu, yalishatokea kwa Kanye, kwa Mr Bizness, unaona bwana, hiyo ni kawaida. Nimeweza kuexpress pia kile ambacho mimi nafeel, nafikiri that’s hip hop yaani nini kile kilichonitokea mimi, nimekiexpress watu wamekisia wameona.
Kuhusu kupigiwa simu ya vitisho
Hiyo simu nilipigwa baada ya ‘Rizone’ kutoka ilikuwa kama wiki mbili hivi. Simu nilipigwa na private call mimi sikuweza kujua ni nani na ilikuwa ni usiku. Kwahiyo nilitishwa tu vile, ‘wewe unatoa hizi nyimbo unaongea ongea huo ujinga nini nini, utaona sasa na wewe kaa tayari’ si unajua zile. Nikaona hii nayo imetokea mwaka jana kwanini nisiexpress vitu ambavyo vimenitokea mimi.
Katika hatua nyingine Izzo B amesema amemaliza video yake iliyofanywa na kampuni ya E-Media chini ya Nick Dizzo na wiki hii inaweza kutoka.