Jay Mo kuwashirikisha Ay na Mr. Blue kwenye CBM

 

Rapper Jumanne Mchopanga aka Jay Mo ameteam up na P-Funk Majani kumfanyia ngoma mpya atakayowashirikisha Ambwene Yesaya aka AY na Herry Sameer aka Mr. Blue kwenye ngoma iitwayo CBM.

Akiongea jana na East Africa Radio, Jay Mo amesema lengo la kufanya ngoma hiyo ambayo kirefu chake ni Check Bob Maarifa ni kuleta kumbukumbu iliyosaulika.

 

Alisema enzi hizo wakati muziki wa kizazi kipya ndo umeanza kupamba moto alikuwepo jamaa aitwaye Slim aliyekuwa akitengeneza nguo ziiitwazo CBM.

Slim ndiye aliyekuwa akilidhamini kundi la CBM lililokuwa likiundwa na AY, Snare na Buff G na anakumbukwa kwa mchango wake kwa wasanii wengi nchini Tanzania.

Jay Mo amesema kuwa ndio maana amemshirikisha AY anayeijua vizuri CBM na Mr. Blue ambaye ni definition halisi  ya Check Bob Maarifa.
 

Ameongeza kuwa Mr. Blue ambaye bado hajaingiza verse zake anaweza kuwafunika wote kutokana na uwezo mzuri alionao.

Kama mambo yakienda sawa wimbo huo utatoka hivi karibuni.