KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS 2013

Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013 zimezinduliwa leo rasmi ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa nembo yake na kusaini mkataka na BASATA wa udhamini kwa miaka mitano. Mdhamini mkuu ni kampuni ya bia Tanzania-TBL kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro Lager. Kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni nne za kitanzania zitatumika ndani ya miaka mitano katika zoezi zima za Tuzo hizi kubwa barani Africa.

Tuzo hizi kwa mwaka huu zinatarajiwa kufanyika tarehe 8 June 2013 katika ukimbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Kwa habari zaidi na matukio ya picha kuhusu uzinduzi wa tuzo hizi tembelea BONGO5 katika link hii: www.bongo5.com/picha-tuzo-za-kili-music-zazinduliwa-rasmi-03-2013/ //JANB MULTIMEDIA