Kim Kardashian kuhost show ya 2face, Flavour na Ice Prince jijini Lagos

Mchumba wa rapper Kanye West, Kim Kardashian anatarajiwa kutua nchini Nigeria mwezi huu.

Mrembo huyo na staa wa Reality TV show atakuwa mshereheshaji mwenza pamoja na msanii wa Darey kwenye concert maalum ya Valentine’s Day iliyopewa jina la  ‘Love Like a Movie’ itakayofanyika February 17 jijini Lagos kwenye kiota cha Eko Hotel and Suites.

Wasanii wengine watakaotumbuiza kwenye show hiyo ni pamoja na Iyanya, Darey, Timi Dakolo, Waje, 9ice, Praiz, Naeto C na kundi la Afrika Kusini Jozi.

Hivi karibuni Kim aliitembelea nchini Ivory Coast.