Lulu apanga kuongea na waandishi wa habari

Baada ya kutoka nje kwa dhamana kwa kesi ya kuua bila kukusudia, muigizaji wa filamu Elizabeth Michael aka Lulu, anatarajia kuongea na waandishi wa habari hivi karibuni.

Kwa mujibu wa muigizaji mwenzie, Dr Cheni press conference hiyo itafanyika siku si nyingi lakini hakuweza kutaja tarehe.

Lulu alitoka kwa dhamana ya shilingi milioni 40. Anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia Steven Kanumba.

Hivi karibuni yeye na mama yake walitembelea kaburi la muigizaji huyo.