Maambukizi ya VVU (HIV) 2011/2012-TANZANIA

Data za TACAIDS kuhusiana na maambujkizi ya VVU (HIV) kwa mwaka 2011/2012:
Mikoa 10 inyoongoza kwa maambukizi ya VVU (HIV):
1. Njombe (14%) 2. Iringa (9.1%) 3. Mbeya (9%) 4. Mara (7.5%) 5. Ruvuma (7%) 6. Dar es Salaam (6.9%) 7. Rukwa (6.2%) 8. Katavi (5.9%) 9. Pwani (5.9%) na 10. Tabora (5.1)
Mikoa 5 inayoongoza kwa mwanaume mmoja kutembea na zaidi ya wanawake watano: 1. Geita (32%) 2. Lindi (30%) 3. Dar es Salaam (29%) 4. Iringa (27%) na 5. Mtwara (22%)
Mikoa 5 inayoongoza kuwa na wanaume wasiotahiriwa ni:
1. Njombe (49%) 2. Katavi (44%) 3. Kagera (39%) 4. Mbeya (38) na 5. Rukwa (28%).
Kwa mujibu wa utafiti, hali ya maambukizi imepungua ambapo idadi ya watu na maambukizi ni asilimia 5.1 kutoka 5.8 ya mwaka 2008.
Umejifunza nini? Maoni yako ni nini? Je, wewe ni miongoni mwa wapambanaji dhidi ya maambukizi VVU (HIV)?