Maandalizi ya Redd's Miss Ubungo yazidi kupamba moto

Mashindano ya Urembo ya Redd’s Miss Tanzania 2012 yanaendelea kwa kasi kubwa na kwa wiki hii kutakuwa na shindano moja kubwa hapa jijini Dar es salaam ambapo kituo cha Ubungo yaani “REDD’S MISS UBUNGO 2012” kitakuwa kikifanya shindano lake.

Shindano hili litafanyika Ijumaa hii ya tarehe 29 / 06 / 2012 katika Ukumbi wa Hotel ya LANDMARK iliyopo ubungo kuanzia saa mbili usiku..

kiingilio katika shindano hili kimepangwa kuwa tsh. 10,000/= tu na burudani itakayosindikiza shindano hili itatoka kwa bendio ya FM ACADEMIA (wazee wa ngwasuma)

kituo hiki cha miss ubungo ndicho kilichomtoa Miss Tanzania 2004 FARAJA KOTTA, hivyo ni mategemeo yetu tutatoa tena Miss Kinondoni na hatimae ndie atakaekuwa REDD’S MISS TANZANIA 2012.

Jumla ya warembo kumi na sita wamejitokeza kuwania taji hili wakiwa chini ya mwalimu wao BEATRICE JOSEPH ambaye alikuwa Miss Ruvuma 2004 na kwa upande wa shoo ya ufunguzi wanafundishwa na BOKILO ambaye ni mwanamuziki kutoka TOT BAND.

Majina ya washiriki ni yafuatayo:-

1.ASHA MUSA (20) 2. FOTUNE ANDE (22).3.MWATUMU MUSTAPHA (21) 4.ZAWADI GULABA (18)5.LILIAN KENNEDY (21) 6.DALINE MMALY (19)7.AXER PETER (20) 8.NASRA DAFFA (22)9.JOYCE RAPHAEL (20) 10.PRINCES REMMY (20)11. MWANAIDI RAMADHANI (20) 12.ZENA ALLY (18)13. DORICE CHILONGOLA (20) 14.SUZAN STANLEY (21)15.ADAIYA AHMED (22) 16. SAHY PAUL (22)
Shindano hili limedhaminiwa na:-REDD’S, MBEKENYELA TRANSPORT, LADY PEPETA, FLEXIP, NAEEMS CLASSIC WEAR na CLOUD’S FM.

SOURCE: https://magangaone.blogspot.com/