Missy Elliot aishitaki kampuni ya kuuza magari

Rapper na producer Missy Elliot anaishtaki kampuni ya kuuza magari ya jimboni Illinois kwa madai kuwa gari lake aina ya Lamborghini brand new linashikiliwa na kampuni hiyo licha ya kuwalipa hela ili kupewa gari lake.

Rapper huyo ameandikisha kesi yake jimboni Florida dhidi ya kampuni ya Fox Valley Motor Cars, akidai kuwa aliingia makubalino na kampuni hiyo mwaka jana kununua mkoko huo ya kifahari, 2012 Matte White Lambo Aventador wenye thamani ya $376,000.

 

Kwa mujibu wa shtaka hilo, Missy – anayewakilishwa na Singh, Singh & Trauben alikubali kulipa advance ya $30,000 cash pamoja na kuwapa gari lake 2005 Bentley (lenye thamani ya $85,000).

Kwa makubaliano hayo, Missy anadai kampuni hiyo ilitakiwa kumtumia gari hilo katikati ya mwaka huu lakini haikufanya hivyo.

Missy anasema aliwasiliana na Fox Valley kupata maelezo lakini aliambiwa kuwa vigezo vimebadiika kwasababu bei ya gari hilo imeongezeka sokoni.

 

Kwa mujibu wa maelezo yake, Fox Valley ilikataa kumpa gari lake kutokana na kupanda kwa bei yake na ikadai iongezewe hela zaidi.

Lakini Missy anasema huo ni upuuzi na sasa anaishtaki kampuni hiyo kwa kung’ang’ania Lambo yake na pia akiitaka imlipe hasara inayotokana na kuvunjwa kwa mkataba huo.