Mtoto wa kambo wa Usher mahututi kwa kugongwa na boti

 

Mtoto wa kambo wa Usher ambaye mama yake ni Tameka Foster, mke wa zamani wa Usher, yupo mahututi baada ya kugongwa na boti (jet ski) kwenye ziwa Lanier huko Georgia Marekani.

Mtoto huyo mwenye miaka 11, Kyle Glover anaidaiwa alikuwa amekaa kwenye tube iliyokuwa ikivutwa na boti kwenye ziwa hilo akiwa na msichana mwenye miaka 15 ambaye hajulikani na ndipo walipogongwa kichwani na Jet ski hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na mwanaume wa miaka 38.

Watoto hao walipelekwa kwa ndege kwenye hospitali ya watoto ya Egelston mjini  Atlanta.

Ingawa Usher na Tameka bado wapo kwenye mgogoro juu ya taraka yao na umiliki wa watoto, mwanamuziki huyo alikodi ndege kumfuta Tameka alikokuwa ili awe karibu na mwanae.

Watu maarufu akiwemo Russell Simmons na Fantasia wamewapa pole Usher na Tameka kwa tukio hilo kupitia Twitter.

Russell alitweet "Praying that Usher and Tameka's son is OK..."

Wakati Fantasia akisema :"Everyone PLEASE pray for Usher and Tameka's son! This is the time they really need your prayers!"