Muigizaji maarufu wa Nollywood Justus Esiri afariki dunia

Nollywood  na tasnia nzima ya burudani ya Nigeria imepata pigo baada ya kuondokewa na muigizaji mahiri na mkongwe wa filamu Justus Esiri.

Esiri alifariki dunia juzi February 19, 2013.

Miongoni mwa watoto wa muigizaji huyo ni msanii  Sidney ‘Dr SID’ Esiri  ambaye alipost picha ya baba yake kwenye Twitter na kuandika ‘RIP Dad‘.

Esiri aliaza kuigiza tangu miaka ya 70 na ameacha mke na watoto sita.