Nahreel na Aika watoka na track yao, ni baada ya kujitoa Pahone

Baada ya kujitoa kwenye kundi la Pahone, Nahreel na mpenzi wake Aika wameachia ngoma yao iitwayo Usinibwage.

Producer huyo maarufu nchini na aliyekuwa member wa kundi la Pahone na Aika wamejitoa kwenye kundi hilo kwa kudai kuwa wameshindwa kuelewana kama kundi na ugomvi wa kila siku.

Aika alisema licha ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Nahreel kila mmoja ataendelea kuwa solo artist.

Alisisitiza kuwa yeye sio sababu ya kuvunjika kwa kundi hilo.

Sikiliza wimbo wao hapa: https://www.sammisago.com/2013/02/skiliza-wimbo-wa-aika-na-nahreel.html?spref=tw