Navio amlilia Goldie

Staa wa muziki nchini Uganda, Navio ni miongoni mwa watu walioumizwa zaidi na taarifa za kifo cha mwakilishi wa mwaka jana wa Nigeria kwenye shindano la Big Brother Africa, Goldie Harvey.

Navio ambaye ameshafanya wimbo na Goldie uitwao Kamili ametumia mitandao ya Twitter na Facebook kuelezea huzuni yake.

“My little sister has passed away. Goldie Harvey honourably Represented Nigeria in the Big Brother House, and was on the fast track to changing the Industry. She believed in a bigger Africa, that went beyond her own borders. Goldie Harvey was an inspiration to me. And will always be my little sis. Rest in Peace Babe,” ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.

“@GoldieHarvey We miss you already. You were about to change Africa in ways we can't even understand now. You are my sister, always,” ametweet.

Goldie amefariki jana usiku nchini Nigeria.