Prezzo aondoka Nigeria kufuatia vitisho anavyopokea baada ya kifo cha Goldie

Baada ya kwenda Nigeria kukutana na aliyekuwa mpenzi wake marehemu Goldie Harvey na kukutana na habari mbaya ya kifo chake, rapper Prezzo amelazimika kuondoka nchini Nigeria kurejea nyumbani nchini Kenya kufuatia vitisho alivyovipata kutoka kwa mtu anayesema ni mume wa Goldie, Andrew Harvey.

Kupitia Facebook Andrew Harvey alimtishia Prezzo kwa kuandiak, “Leave our family to grieve in peace… You have already caused us enough pain.”

Kufuatia vitisho hivyo Prezzo ameifupisha ziara safari yake nchini humo na huenda asihudhurie mazishi ya Goldie.